Burnley Yapanda Ligi Kuu ya Uingereza

Nahodha wa Burnley, Josh Brownhill, aliirejesha timu yake Ligi Kuu ya England kwa kufunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Sheffield United, ushindi uliowapa pia Leeds tiketi ya kupanda daraja, huku Sheffield wakibaki kutegemea mechi za mchujo (play-offs).

Burnley Yapanda Ligi Kuu ya Uingereza

Scott Parker alitimiza mafanikio ya kupandisha timu daraja kwa mara ya tatu akiwa na vilabu vitatu tofauti ndani ya misimu sita, huku Burnley wakivunja rekodi yao kwa kutopoteza mechi 31 mfululizo kwenye ligi  na kurejea Ligi Kuu mara moja kama walivyofanya baada ya kushushwa daraja mwaka 2015 na 2022.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Brownhill aliifungia Burnley bao la kwanza baada ya shuti la Josh Cullen dakika ya 28 kuokolewa na kipa.

Hata hivyo, Burnley hawakuweza kuweka rekodi ya “clean sheet” ili kulingana na rekodi ya Port Vale ya mechi 30 bila kuruhusu bao katika msimu mmoja, kwani Tom Cannon alisawazisha haraka kwa upande wa Sheffield. Lakini Brownhill aliwarejesha tena Burnley mbele kupitia penalti kabla ya mapumziko likiwa bao lake la 16 msimu huu.

Burnley Yapanda Ligi Kuu ya Uingereza

Ushindi huo uliifanya Burnley kusawazisha alama na Leeds kileleni mwa msimamo, zote zikiwa na nafasi ya kumaliza msimu na pointi 100. Lakini kwa Sheffield, ambayo imepoteza mechi nne kati ya tano zilizopita, walilazimika tena kwenda kwenye mchujo.

Sheffield United imewahi kushiriki mechi za mchujo mara nane, ikifika fainali nne, lakini bado haijawahi kupanda daraja kupitia njia hiyo.

Vijana wa Chris Wilder waliwasili mashariki mwa Lancashire wakijua njia pekee ya kuendelea kupigania kupanda moja kwa moja ilikuwa ni kuwa timu ya kwanza msimu huu kushinda kwenye uwanja wa Turf Moor  na hakika walikuja na nia hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.