Mkurugenzi wa zamani wa Barcelona na Milan, Ariedo Braida, anaamini kuwa Inter wanaweza kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. “Barcelona wanapigika,” amesema.

Tumeingia katika hatua ya nne bora ya michuano mikubwa kabisa ya vilabu barani Ulaya, ambapo Arsenal watacheza dhidi ya Paris Saint-Germain katika nusu fainali moja, huku Inter wakiwakabili Blaugrana katika Nusu Fainali nyingine.
Kuelekea mchezo wa kwanza utakaopigwa kwenye uwanja wa Olimpiki Lluis Companys mnamo Aprili 30, Radio Anch’Io Sport ilizungumza na Braida, aliyewahi kuwa mkurugenzi wa Milan na Barcelona, kutaka maoni yake kuhusu michuano hiyo.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
“Katika nyakati zangu, Barcelona walikuwa timu ya kutisha. Sasa bado ni timu nzuri, lakini wanaweza kupigika. Ulinzi wao si mgumu sana kuvuka. Hata hivyo, kwenye safu ya ushambuliaji wana wachezaji wa kiwango cha juu, wanaweza kuibua kitu chochote hata katika wakati mgumu zaidi.” Alijibu Braida.


