Walcott Amshauri Eberechi Eze Kuhusu Kujiunga na Arsenal

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Theo Walcott, amemtaka Eberechi Eze kuwa makini na uamuzi wa mustakabali wake, akisisitiza kwamba kubaki Crystal Palace huenda kukawa chaguo bora zaidi endapo anataka nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha England kitakachoshiriki Kombe la Dunia mwakani.

Walcott Amshauri Eberechi Eze Kuhusu Kujiunga na Arsenal

Eze, mwenye umri wa miaka 27, aliweka alama kubwa msimu uliopita baada ya kufunga bao la ushindi kwenye fainali ya kihistoria ya FA Cup dhidi ya Manchester City katika Uwanja wa Wembley mwezi Mei. Jumapili iliyopita, alirejea tena Wembley na kusaidia Palace kutwaa Community Shield kwa kuwashinda Liverpool kupitia mikwaju ya penalti.

Hata hivyo, kumekuwa na tetesi kwamba Eze anaweza kuondoka Selhurst Park kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Premier League, huku Tottenham Hotspur na Arsenal zikiripotiwa kumwania. Ingawa anadaiwa kufurahishwa na wazo la kujiunga na Spurs, taarifa zinaonyesha angependelea zaidi kuhamia Arsenal ikiwa dili litafungwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Mkataba wake una kipengele cha kuachwa kwa dau la pauni milioni 68, kinachodumu hadi Ijumaa hii.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Walcott Amshauri Eberechi Eze Kuhusu Kujiunga na Arsenal

Akizungumza kwenye podcast ya It’s Called Soccer, Walcott alisema:

“Ni mwaka wa Kombe la Dunia, na kama mchezaji, nafikiria ‘nitaichezea Palace kila wiki’. Ukienda Arsenal, shinikizo ni tofauti, wanapigania ubingwa na kuna mazungumzo mengi kwamba Mikel Arteta anatakiwa kushinda kitu mwaka huu. Eze ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee, atasaidia kikosi, lakini swali ni je, itamsaidia yeye binafsi?”

Walcott Amshauri Eberechi Eze Kuhusu Kujiunga na Arsenal

Walcott aliongeza kuwa Palace inampa Eze uhuru wa kucheza kwa maverick style yake, na kujaribu mambo mapya uwanjani, kitu ambacho huenda asikipate akihamia Arsenal, ambapo ushindani wa namba na matarajio makubwa huenda yakampunguzia nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.