Barcelona Kumlinda Olmo Baada ya Msimu Uliojaa Majeraha

Barcelona wameamua kumuangalia Dani Olmo kwa tahadhari ya hali ya juu, kufuatia msimu wa 2024/25 uliosheheni changamoto za majeraha yaliyomnyima ubora wake wa uwanjani, kwa mujibu wa ripoti ya Pau Bartoli kupitia SPORT.

Barcelona Kumlinda Olmo Baada ya Msimu Uliojaa Majeraha

Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alikosa jumla ya mechi 15 msimu uliopita, ikiwemo ile muhimu ya marudiano ya nusu fainali ya Copa del Rey dhidi ya Atletico Madrid, ambapo uwepo wake ungeweza kuleta mabadiliko makubwa.

Ingawa hakuna jeraha lililokuwa kubwa, matatizo ya mara kwa mara hasa muscle overloads na maumivu madogo yalikatisha kasi yake na kumlazimisha kocha Hansi Flick kubadilisha mipango. Flick amesisitiza kwamba afya ya wachezaji inabaki kuwa kipaumbele, hususan kwa mchezaji muhimu kama Olmo katika mfumo wake wa kiufundi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Barcelona Kumlinda Olmo Baada ya Msimu Uliojaa Majeraha

Msimu mpya tayari umetoa onyo la mapema. Wakati wa maandalizi ya msimu, Olmo alipata tena maumivu ya misuli yaliyomnyima mazoezi kadhaa wiki iliyopita na kumfanya aikose Joan Gamper Trophy dhidi ya Como. Bahati nzuri, hali hiyo haikuwa mbaya, na alirejea mazoezini kikamilifu Jumanne, akitarajiwa kuwepo kwenye mechi ya ufunguzi wa La Liga dhidi ya Mallorca Jumamosi.

Hata hivyo, tukio hilo limetilia mkazo haja ya kuwa makini zaidi katika kudhibiti ratiba yake. Timu ya kitabibu na benchi la ufundi sasa wapo mbioni kuunda mpango maalum wa mazoezi utakaolingana na mwili wake na kupunguza hatari ya kuumia mara kwa mara. Lengo ni kumpa uthibiti utakaomwezesha kudumu katika kiwango cha juu msimu mzima.

Barcelona Kumlinda Olmo Baada ya Msimu Uliojaa Majeraha

Swali linalosalia ni kama Flick atamwamini kuanza dhidi ya Mallorca, au ataendelea na Fermin Lopez, aliyewavutia mashabiki kwa kufunga mabao mawili dhidi ya Como.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.