Alcaraz Na Rekodi ya Ushindi, Aendelea Kung’ara Cincinnati

Carlos Alcaraz ameendelea kuthibitisha ubora wake kwenye mchezo wa tenisi baada ya kuwa mchezaji wa kwanza mwaka huu kufikisha ushindi wa mechi 50, akimchapa Hamad Medjedovic kwa seti 6-4, 6-4 kwenye Cincinnati Masters.

Alcaraz Na Rekodi ya Ushindi, Aendelea Kung’ara Cincinnati

Mchezo huo ulionekana kumtesa mpinzani wake, huku Alcaraz akibaki mtulivu na kutumia mbinu sahihi katika nyakati muhimu. Ushindi huu unaongeza kasi yake kuelekea fainali inayotarajiwa kupigwa Jumapili dhidi ya mpinzani wake mkubwa, Jannik Sinner.

“Nafahamu yeye ni mchezaji mwenye nguvu kubwa, na shots zake ni ngumu sana kuzirudisha. Ana serve kubwa pia. Najua hapendi kukimbia sana kulia na kushoto, kwa hiyo mpango wangu ulikuwa kumfanya akimbie kadri iwezekanavyo,” alisema Alcaraz. “Ilikuwa ngumu kwa sababu mpira wake unaruka na kuja kwa kasi sana, lakini nafurahi kuwa nilifanikiwa mara nyingi na kutetea vizuri.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Alcaraz Na Rekodi ya Ushindi, Aendelea Kung’ara Cincinnati

Wiki hii inampa Alcaraz nafasi kubwa ya kupunguza pengo kwenye viwango vya ATP Rankings, kwani Sinner anatetea pointi 3,500 baada ya kutwaa ubingwa wa Cincinnati Masters na US Open mwaka jana. Alcaraz, kwa upande wake, anatetea pointi 60 pekee kutokana na kutolewa mapema kwenye mashindano hayo mwaka 2024.

Mwaka jana, Alcaraz alitwaa mataji mawili ya Grand Slam French Open na Wimbledon na kumaliza na ushindi wa mechi 54, idadi iliyopunguzwa na majeraha na kuporomoka kwa kiwango mwishoni mwa msimu. Hata hivyo, mwaka huu anaonekana kujipata kwa muda sahihi kuelekea US Open.

Alcaraz Na Rekodi ya Ushindi, Aendelea Kung’ara Cincinnati

Mbali na ndoto ya kutwaa taji Cincinnati, Alcaraz pia atashirikiana na Emma Raducanu kwenye michuano mipya ya mixed doubles US Open, ikitarajiwa kuwa moja ya jozi zinazosisimua zaidi. Baada ya hapo, macho yake yatakuwa kwenye lengo kubwa, kutwaa US Open na kukaribia nafasi ya namba moja duniani kabla ya kufunga pazia la mwaka wa tenisi 2025.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.