Khephren Thuram amefichua jinsi anavyohisi kukutana na kaka yake Marcus uwanjani na kwa nini anaamini baba yao, Lilian Thuram, ataishangilia Juventus dhidi ya Inter. “Familia yetu yote itakuwa jukwaani.”

Mashabiki wasioegemea upande wowote watatarajia kuona marudio ya mechi ile ya kusisimua iliyoisha kwa ushindi wa 4-3 kwa Juventus katika dakika za nyongeza, ambapo ndugu wote wawili wa Thuram walifunga mabao.
“Unapokua na kaka anayependa kucheza mpira wa miguu, ni kawaida kutamani kila wakati muwe timu moja Italia.Shuleni, tulikuwa tukichaguana kwanza kila mara kuingia katika timu zetu. Lakini sasa sisi ni wachezaji wa kulipwa, tunachezea klabu kubwa za Italia, na hilo pia ni jambo zuri. Natumaini kucheza naye mechi nyingi zaidi tukiwa na timu ya taifa ya Ufaransa”. Khephren aliiambia Sky Sport
Mchezaji huyo amesema kuwa anatarajia mchezo mkubwa, kwa sababu hizi ni timu mbili kubwa, zote zinacheza vizuri na zina nguvu kimkakati. Itakuwa mechi ngumu kwa pande zote.
“Tunazungumza kila siku, lakini kamwe si kuhusu mechi. Tunajadili mambo muhimu zaidi kuliko mpira. Hata hivyo, familia yetu yote itakuwa jukwaani safari hii.”

Ni hali inayoweza kumweka baba yao, Lilian beki wa zamani wa Juventus na Parma katika wakati mgumu wa kuchagua upande. Hata hivyo, Khephren ana wazo la kwa nini huenda baba yao akaonyesha tabasamu zaidi kwa upande wa Bianconeri.
“Atakuwa hana upande, lakini mimi ndiye mtoto wa mwisho, kwa hiyo labda atanipa umakini kidogo zaidi”. Juventus imeimarika sana tangu Luciano Spalletti achukue nafasi ya Igor Tudor. Je, kocha huyo anatofautianaje na mtangulizi wake?
Ananiomba niwe ninasogea kila wakati, nitangulie mchezo, lakini jambo muhimu zaidi ni kucheza kwa kujiamini na kujua kwamba nina nguvu.Ni mmoja wa makocha ambao katika maisha yangu ya soka amejaribu zaidi kunifanya nitambue uwezo wangu. Nafurahia kufanya kazi naye. Pia hunipa ushauri kuhusu maeneo ninayopaswa kuboresha, lakini nitayaweka hayo binafsi. Alisema Khephren Thuram.
Spalletti anadai mengi kutoka kwa timu, anatuhitaji tufanye mambo mengi, nasi tunajitahidi kumridhisha. Alinalizia mchezaji huyo.