Mourinho Afunguka Tetesi za Kurejea Real Madrid

Kocha wa SL Benfica, Jose Mourinho, anajiandaa kwa mchezo mkubwa wa mchujo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid, katika mechi inayobeba hisia kali kwake binafsi. Huku jina lake likitawala vichwa vya habari kabla ya pambano hilo, tetesi zimekuwa zikiongezeka kuhusu uwezekano wa kurejea Santiago Bernabeu.

Mourinho aliinoa Real Madrid kati ya mwaka 2010 hadi 2013, akivunja utawala wa Barcelona kwa kutwaa taji la La Liga kwa alama 100, rekodi iliyotikisa Hispania wakati huo. Urithi wake Madrid umebaki kuwa wa mafanikio makubwa yaliyochanganyika na ushindani mkali wa hali ya juu.

Mourinho Afunguka Tetesi za Kurejea Real Madrid

Kutokana na uvumi kuwa rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, huenda anatafuta kocha mwenye uzoefu wa ushindi ili kuiongoza timu katika kipindi cha mpito, Mourinho aliulizwa moja kwa moja kuhusu uwezekano wa kurejea. Kwa kawaida yake ya uwazi, alikiri kuwa bado ana hisia maalum kwa klabu hiyo.

“Nilitoa kila kitu kwa Real Madrid. Nilifanya mazuri na mabaya, lakini nilitoa kila nilichokuwa nacho,” alisema. “Niliondoka miaka 12 iliyopita, lakini bado ninapokutana na mashabiki wa Madrid popote duniani, kuna hisia ileile, kwamba nilitoa kila kitu kwa klabu.”

Mourinho Afunguka Tetesi za Kurejea Real Madrid

Uvumi huo pia umechangiwa na taarifa kuwa Mourinho ana kipengele maalum katika mkataba wake na Benfica kinachorahisisha kuvunja mkataba. Hata hivyo, aliweka wazi kuwa kipengele hicho kililenga kulinda maadili wakati wa kipindi cha uchaguzi wa klabu, ili kutoa uhuru kwa pande zote iwapo kungekuwa na mabadiliko ya uongozi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mourinho Afunguka Tetesi za Kurejea Real Madrid

“Sitaki kulisha hadithi zisizokuwepo. Kitu pekee kilichopo ni kwamba nina mwaka mmoja zaidi wa mkataba na Benfica,” alisisitiza. “Ndiyo, kuna kipengele kinachorahisisha kuvunja mkataba kwa pande zote, lakini kwa sasa nina mkataba na Benfica. Na kuhusu Real Madrid, hakuna chochote.”

Kauli hiyo imeweka wazi msimamo wa Mourinho, angalau kwa sasa, huku macho ya mashabiki yakielekezwa kwenye pambano la leo lenye uzito mkubwa barani Ulaya.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.