Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kucheza michezo mitatu mfululizo ugenini katika mwezi huu wa Machi kwenye mashindano ya Ligi Kuu ya NBC, kufuatia ratiba iliyothibitishwa rasmi na klabu hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Mnyama ataanza safari yake ya ugenini Machi 11 kwa kumenyana na Singida Black Stars katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mchezo huo utakuwa kipimo muhimu kwa wekundu hao wa Msimbazi katika harakati zao za kuwania ubingwa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Baada ya hapo, Machi 14, Mnyama atasafiri kucheza dhidi ya TRA united FC , kabla ya kuhitimisha mfululizo huo wa mechi za ugenini Machi 19 kwa kukutana na Pamba Jiji FC ya Mwanza

Ratiba hiyo inaipa Simba changamoto ya kucheza michezo yote mitatu nje ya nyumbani ndani ya kipindi kifupi, jambo linalohitaji maandalizi makini ya kiufundi na kimwili ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya.

Mashabiki wa Simba wanatarajia kuona timu yao ikifanya vyema katika michezo hiyo muhimu, huku kila pointi ikiwa na uzito mkubwa katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu,

