Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, ameibua sintofahamu kuhusu mustakabali wa Antoine Griezmann huku kukiwa na uwezekano wa nyota huyo kuondoka kabla ya fainali ya Copa del Rey. Licha ya kiwango bora cha Mfaransa huyo msimu huu, tetesi za kujiunga na klabu ya MLS, Orlando City SC, zimezua mjadala mkubwa ndani na nje ya klabu hiyo ya Madrid.

Atletico walitinga fainali baada ya kuiondoa FC Barcelona kwa ushindani mkali. Griezmann alikuwa kiungo muhimu wa mafanikio hayo, akiongoza mashambulizi na kuwa mhimili wa kiufundi wakati timu ikiwa chini ya presha kubwa. Hata hivyo, nyuma ya pazia, mazungumzo yanayomhusisha na MLS yanaendelea kuripotiwa kushika kasi, hali inayotia shaka uwepo wake kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa mwezi ujao.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Griezmann chini ya Simeone hajatwaa taji kubwa na Atletico tangu ushindi wa UEFA Super Cup mwaka 2018, jambo linalofanya safari ya msimu huu kuwa ya kihisia kwake binafsi. Kwa mujibu wa ripoti, Orlando City wanataka kumshawishi ajiunge nao kabla dirisha lao la usajili kufungwa Machi 26, ingawa inaelezwa kuwa ana uwezekano mkubwa wa kusubiri hadi dirisha la kiangazi kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho.
Baada ya ushindi wa nusu fainali, Diego Simeone hakuficha hisia zake. Alikiri kuwa anatumaini kumuona Griezmann akicheza fainali, akisisitiza kuwa anastahili zaidi ya yeyote. Nahodha wa timu, Koke, naye alikubali kuwa wachezaji hawajui hatma ya mwenzao huyo, akisisitiza kuwa uamuzi ni wake binafsi licha ya tamanio la wengi kumaliza soka lake Atletico.

Wachezaji wengine kama Marcos Llorente na Juan Musso wameeleza heshima yao kwa mchango wa Griezmann na kuahidi kumuunga mkono kwa uamuzi wowote atakaofanya. Ndani ya kikosi hasa kwa Simeone kuna hali ya kukubali kwa shingo upande, wakijua kuwa wanaweza kumpoteza gwiji wao katika wakati muhimu zaidi wa msimu lakini pia wakiheshimu ndoto na malengo yake binafsi.

