Kocha wa Liverpool FC Slot, amekiri kuwa Liverpool lazima washughulikie tabia yao ya kupoteza mabao mwishoni mwa michezo ili kuokoa msimu wao mgumu, baada ya kufungwa 2-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers, ambao wako katika nafasi ya mwisho ya ligi ya EPL.

Slot amesema timu yake ilikuwa mbali na mpangilio bora katika sehemu ya kwanza ya mchezo, huku sehemu ya pili ikionyesha juhudi zaidi za kufunga, lakini walipoteza bao baada ya mpira wa Andre kubadilika mwelekeo na kuingia kwenye lango la kipa Alisson Becker.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo ameleza kuwa Liverpool walitengeneza nafasi chache kuliko wapinzani wao lakini bado matokeo yalibaki hasara, akisisitiza kuwa tabia ya kupoteza mabao katika dakika za mwisho ni tatizo linalohitaji suluhisho haraka kabla ya kuhitimisha mojawapo ya misimu isiyofaa katika historia ya klabu hiyo.


