Presha imezidi kupanda kwa Alvaro Arbeloa ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu, huku ripoti kutoka Italia zikidai kuwa rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, tayari anatazama mbadala wa benchi la ufundi. Baada ya kuondoka kwa Xabi Alonso, Madrid wamepitia kipindi kigumu, na licha ya Arbeloa kujitahidi kuziba pengo hilo, uongozi unaonekana kutoridhishwa na mwelekeo wa sasa wa timu.

Kipigo cha 1-0 nyumbani dhidi ya Getafe CF kimezidisha hali ya sintofahamu, huku Madrid wakibaki nyuma kwa alama nne dhidi ya FC Barcelona katika mbio za ubingwa wa La Liga. Nidhamu imekuwa tatizo, na kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kinda Franco Mastantuono imeongeza maumivu kwa kikosi hicho. Arbeloa mwenyewe alikiri akisema kuwajibika kuboresha uchezaji ni jukumu lake.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Italia, Madrid wanamfikiria kwa uzito kocha wa AC Milan, Massimiliano Allegri, kwa ajili ya msimu wa 2026-27. Allegri ana mkataba hadi 2027 katika dimba la San Siro, lakini uzoefu wake, mbinu zake za kimkakati na uwezo wa kushughulika na presha ya klabu kubwa vinatajwa kuwa sababu kuu zinazomvutia Perez.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hii si mara ya kwanza kwa Allegri kuhusishwa na kazi hiyo yenye hadhi kubwa barani Ulaya. Inaripotiwa kuwa aliwahi kufikia makubaliano ya maneno na Madrid mwaka 2021 kabla ya kubadili uamuzi na kurejea Juventus FC kufuatia mazungumzo na rais wa wakati huo, Andrea Agnelli. Sasa, inaonekana nyota zinaweza kuungana tena kwa ajili ya hatua hiyo.
Ingawa jina la Jurgen Klopp limekuwa likitajwa kama chaguo la kuvutia, kocha huyo kwa sasa yuko katika majukumu yake mapya ndani ya mtandao wa Red Bull na hana dalili ya kurejea haraka kwenye benchi. Hivyo basi, iwapo Madrid wataamua kuvuta kigingi kwa Arbeloa, Allegri anaonekana kuwa chaguo sahihi akiwa kocha mwenye uzoefu wa kushinda mataji.

