TFF Yatoa Ufafanuzi Hatua za Utekelezaji wa VAR Nchini

Afisa Habari wa Shirikisho la Mpila wa Miguu Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, ametoa ufafanuzi kuhusu changamoto na hatua zinazoendelea katika utekelezaji wa teknolojia ya Video Assistant Referee (VAR) nchini, akieleza kuwa mchakato huo unahitaji maandalizi ya kina na mafunzo maalumu kwa waamuzi.

Ndimbo amesema matumizi ya VAR hayawezi kuanza mara moja kwenye mechi bila kufuata taratibu zilizowekwa na FIFA, kwani waamuzi wanapaswa kupitia mafunzo maalumu yenye ngazi sita (module 6) kabla ya kupewa kibali cha kutumia teknolojia hiyo.Kwa mujibu wa Ndimbo, hadi sasa Tanzania imefanikiwa kukamilisha ngazi nne za mafunzo huku mbili zikiwa bado, na mafunzo hayo yanaendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA ambao wanatoa mwongozo na usimamizi wa karibu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

TFF Yatoa Ufafanuzi Hatua za Utekelezaji wa VAR Nchini
Alieleza kuwa waamuzi wa Tanzania tayari wanaendelea kushiriki katika kozi hizo na kwamba TFF pia Linasubiri kukamilika kwa hatua zote muhimu kabla ya kuanza rasmi kutumia VAR katika mechi.“Ukimaliza mafunzo yote ndipo unakuwa umehitimu kuanza kutumia VAR, na hata baada ya hapo unapaswa kupewa kibali kinachoeleza asilimia ya mechi ambazo unaweza kutumia teknolojia hiyo,” alisema Ndimbo.

TFF Yatoa Ufafanuzi Hatua za Utekelezaji wa VAR Nchini

Aidha, alibainisha kuwa mchakato huo ni wa muda mrefu kwa sababu unahusisha mafunzo kwa waamuzi wote wanaoshiriki katika uendeshaji wa mechi, wakiwemo waamuzi wa kati, waamuzi wasaidizi wa pembeni pamoja na waamuzi wanaosimamia mfumo wa VAR, ambapo kila mmoja ana jukumu maalumu linalohitaji ujuzi wa kutosha kutoka kwa TFF.

Ndimbo alisisitiza kuwa utekelezaji wa VAR si jambo la haraka bali ni mchakato unaoendelea ambao unahitaji maandalizi ya kitaalamu ili kuhakikisha teknolojia hiyo inatumika kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

TFF Yatoa Ufafanuzi Hatua za Utekelezaji wa VAR Nchini

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.