Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Rodrygo Goes, anatarajiwa kuukosa michuano ya Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Brazil, na huenda akakosekana hadi sehemu kubwa ya msimu wa mwaka 2026, kufuatia kupata jeraha kubwa la goti.

Taarifa rasmi kutoka klabuni hapo zimethibitisha kuwa Rodrygo amepasuka kano ya mbele ya goti (ACL) pamoja na kupata majeraha katika sehemu ya nje ya goti la mguu wa kulia.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Rodrygo alirejea uwanjani Jumatatu katika mchezo uliomalizika kwa Getafe CF kuibuka na ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Real Madrid. Hata hivyo, baada ya kugongana na mpinzani karibu na mstari wa pembeni, alianguka na kushika goti lake mara moja kuashiria maumivu makali. Ingawa aliendelea kucheza kwa takribani dakika 30 zaidi, ilionekana wazi kuwa hakuwa katika hali nzuri kimwili.

Jeraha hilo ni pigo kubwa kwa Real Madrid, ambayo tayari inawakosa wachezaji wengine muhimu akiwemo Kylian Mbappé anayesumbuliwa na maumivu ya goti, pamoja na Franco Mastantuono ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo huo dhidi ya Getafe. Kukosekana kwa Rodrygo kunatarajiwa kuathiri mipango ya klabu hiyo na timu ya taifa ya Brazil katika mashindano yajayo ya kombe la dunia.
Washambuliaji pekee waliobaki wakiwa fiti ni Vinícius Júnior na Gonzalo García, pamoja na Brahim Díaz, ambaye inaonekana hayumo sana katika mipango ya kocha. Real Madrid wapo nyuma kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya FC Barcelona wanaoongoza kileleni mwa La Liga, na wanatarajiwa kukutana na Manchester City katika hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League hivi karibuni.

Wakati huo huo, timu ya taifa ya Brazil inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki katika wiki zijazo dhidi ya Mataifa ya Ufaransa na Croatia kama sehemu ya maandalizi ya Kombe la Dunia.
Hali hiyo itapelekea Kwa Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Carlo Ancelotti sasa atalazimika kupanga upya kikosi chake bila ya mmoja wa wachezaji wake muhimu.


