CAF Yaongeza Fedha za Zawadi Kwa Bingwa wa Klabu Bingwa na Shirikisho

Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF limetangaza kuongeza tena kiwango cha fedha za zawadi kwa mashindano yake ya klabu ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup, ambapo washindi wa kila mashindano sasa wataongezewa dola milioni mbili zaidi.

CAF Yaongeza Fedha za Zawadi Kwa Bingwa wa Klabu Bingwa na Shirikisho

Kwa mujibu wa CAF, bingwa wa michuano ya Klabu bingwa sasa atapata kitita cha dola milioni 6 za Marekani sawa na Tsh B. 16.2, huku mshindi wa kombe la shirikisho akiondoka na dola milioni 4 sawa na Tsh. B 10.8. Ongezeko hilo linaendelea kutekeleza ahadi ya Rais wa CAF Patrice Motsepe ya kuongeza uwekezaji katika mashindano ya klabu barani Afrika.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

CAF imeeleza kuwa kwa sasa inatumia fedha nyingi zaidi katika zawadi na gharama za uendeshaji wa CAF Champions League pekee kuliko ilivyokuwa ikitumia kwa mashindano yote mawili wakati Motsepe alipoingia madarakani mwezi Machi mwaka 2021.

CAF Yaongeza Fedha za Zawadi Kwa Bingwa wa Klabu Bingwa na Shirikisho

Wakati Motsepe anaingia madarakani, bingwa wa CAF Champions League alikuwa akipata dola milioni 2.5, huku mshindi wa kombe la shirikisho akipata dola milioni 1.25 pekee, hali inayodhihirisha ongezeko kubwa la uwekezaji katika mashindano hayo.

Katika hatua nyingine ya kuhamasisha ushiriki wa klabu nyingi zaidi, CAF imeanzisha pia ruzuku kwa timu zinazotolewa katika hatua za awali za mashindano. Ruzuku hiyo ilianza kwa dola 50,000 katika msimu wa 2024/25 na kuongezwa hadi dola 100,000 katika msimu wa 2025/26.

CAF Yaongeza Fedha za Zawadi Kwa Bingwa wa Klabu Bingwa na Shirikisho

Kwa mujibu wa CAF, jumla ya klabu 130 zilishiriki katika mashindano hayo msimu huu ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kutokea, huku uwekezaji wa CAF katika mashindano ya klabu ukiongezeka kutoka dola milioni 18.8 mwaka 2021 hadi kufikia dola milioni 42 msimu huu, wakati hatua ya robo fainali ya mashindano yote mawili ikitarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.