Mashabiki 9 Wakamatwa Baada ya Vurugu Derby ya Rangers na Celtic

Watu tisa wamekamatwa na polisi kufuatia vurugu za mashabiki zilizotokea uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo wa robo fainali wa Scottish Cup kati ya Rangers FC na Celtic FC uliochezwa katika Uwanja wa Ibrox Jumapili.

Mashabiki 9 Wakamatwa Baada ya Vurugu Derby ya Rangers na Celtic

Vurugu hizo zilianza baada ya mashabiki wa Celtic kushangilia ushindi wa timu yao kwa mikwaju ya penalti na kuingia uwanjani, hali iliyosababisha mamia ya mashabiki wa Rangers pia kuvamia uwanja na kusababisha mzozo mkubwa kati ya pande hizo mbili.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Polisi pamoja na walinzi wa uwanja walilazimika kuingilia kati na kuunda ukuta wa kuwazuia mashabiki wa timu hizo mbili, huku baadhi ya mashabiki wakirusha vitu mbalimbali uwanjani ikiwemo mwenge uliokuwa unawaka. Polisi pia wamesema mtoto wa miaka 10 alipigwa na sarafu huku askari mmoja akipigwa kichwani kwa chupa.

Mashabiki 9 Wakamatwa Baada ya Vurugu Derby ya Rangers na Celtic

Picha za video zilizosambaa mitandaoni zilimuonyesha askari mwanamke akipigwa teke na shabiki wa Rangers aliyekuwa akikimbia kuelekea jukwaa la Broomloan lililokuwa na takribani mashabiki 7,500 wa Celtic. Aidha, mwanaume mwenye umri wa miaka 47 alikamatwa baada ya tukio lililomhusisha mmoja wa benchi la ufundi la Celtic.

Mashabiki 9 Wakamatwa Baada ya Vurugu Derby ya Rangers na Celtic

Katika tukio jingine lililonaswa kwa simu za mashabiki, shabiki mmoja alionekana akijaribu kumpiga teke beki wa Celtic Julian Araujo kabla ya mwingine kumsukuma mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico.

Polisi pia walilazimika kukabiliana na vurugu nje ya uwanja ambapo baadhi ya askari, walinzi na raia walijeruhiwa, huku wakisema idadi ya waliokamatwa inaweza kuongezeka zaidi kadri uchunguzi unavyoendelea, jambo lililosababisha mjadala kuhusu kupunguzwa kwa idadi ya tiketi za mashabiki wa ugenini katika derby za jadi kati ya Rangers na Celtic.

Mashabiki 9 Wakamatwa Baada ya Vurugu Derby ya Rangers na Celtic

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.