Rice: Kufika Nusu Fainali Mara Mbili Mfululizo ni Mafanikio Makubwa

Kiungo wa Arsenal FC, Declan Rice, amewajibu wakosoaji baada ya timu yake kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya UEFA Champions League, akieleza kuwa ni “mafanikio makubwa” licha ya sare ya bila kufungana dhidi ya Sporting CP jana Jumatano kwenye dimba la Emirates.

Rice: Kufika Nusu Fainali Mara Mbili Mfululizo ni Mafanikio MakubwaArsenal ilifanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya bao 1-0 kufuatia ushindi walioupata wiki iliyopita ugenini nchini Ureno, ambapo Kai Havertz alifunga bao la ushindi dakika za mwisho. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa timu hiyo kufika hatua ya nusu fainali, baada ya msimu uliopita kutolewa na Paris Saint-Germain ambao baadaye walitwaa ubingwa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika hatua inayofuata, Arsenal itakutana na Atletico Madrid kuwania nafasi ya kufika fainali, ambapo watacheza dhidi ya mshindi kati ya PSG au Bayern Munich mjini Budapest.

Rice: Kufika Nusu Fainali Mara Mbili Mfululizo ni Mafanikio Makubwa“Kurudi tena kwenye nusu fainali mfululizo ni mafanikio makubwa kwa kikosi hiki,” alisema Rice. “Tunataka kwenda hatua moja zaidi ya msimu uliopita na kufika fainali.”

Hata hivyo, mchezo wa sare ya 0-0 haukuwa wa kuvutia sana, hali inayoweka presha kwa kikosi cha kocha Mikel Arteta kuelekea pambano muhimu la Premier League dhidi ya Manchester City mwishoni mwa wiki. Arsenal imeshinda mchezo mmoja tu kati ya mitano iliyopita katika mashindano yote.

Rice: Kufika Nusu Fainali Mara Mbili Mfululizo ni Mafanikio Makubwa“Chanya tu mbele kwa mbele. Nani anajali watu wanasema nini? Kilicho muhimu ni sisi kama kikundi na kocha wetu, na sasa tupo tena nusu fainali. Nimefurahi sana,” aliongeza Rice. “Rekodi yetu msimu huu ni nzuri sana, sasa ni swali la tunataka kiasi gani ushindi. Najua wachezaji wapo tayari, hivyo twende tukapambane.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.