Kane Ampongeza Diaz Baada ya Bayern Kuiondoa Real Madrid Kwenye UCL

Mshambuliaji wa Bayern Harry Kane amempongeza Luis Diaz baada ya mchango wake mkubwa uliosaidia klabu hiyo kuiondoa Real Madrid na kutinga hatua ya nusu fainali ya UEFA Champions League.

Kane Ampongeza Diaz Baada ya Bayern Kuiondoa Real Madrid Kwenye UCLBayern ilikuwa na faida ya mabao 2-1 kutoka mchezo wa kwanza, lakini ilijikuta nyuma mara tatu katika kipindi cha kwanza kutokana na mchezo mkali wa Real Madrid. Hata hivyo, mchezo uligeuka dakika za mwisho baada ya Diaz kufunga bao la ushindi dakika ya 89, kabla ya Michael Olise kuongeza bao la nne katika muda wa nyongeza, na kuifanya Bayern ishinde 4-3 na jumla ya 6-4.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

alisema Kane. “Dakika za mwisho zilihisi kama sisi ndio tulikuwa timu inayotafuta suluhisho zaidi,” “Walianza kuchoka kidogo, na wakati mwingine unahitaji tu moment ya ubunifu, shuti la ajabu au pasi ya kipekee. Hapa Diaz na Olise walifanya kazi kubwa kumaliza mchezo.”

Kane Ampongeza Diaz Baada ya Bayern Kuiondoa Real Madrid Kwenye UCLKane pia alieleza kuwa subira ya kikosi chao ilichangia mafanikio hayo dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria. “Mabadiliko ya hisia katika kipindi cha kwanza yalikuwa ya kipekee, lakini tulibaki kwenye mchezo na tulikuwa na subira. Tulijua kadri muda unavyokwenda tutazidi kuwa bora,” aliongeza.

Bao alilofunga Kane pia limemfanya kuwa mchezaji wa kwanza Mwingereza katika ligi tano bora Ulaya kufikisha mabao 50 katika mashindano yote ndani ya msimu mmoja. “Ni matokeo ya kazi kubwa ya timu nzima, sio mimi peke yangu. Nitaendelea kujituma,” alisema.

Kane Ampongeza Diaz Baada ya Bayern Kuiondoa Real Madrid Kwenye UCLKocha wa Bayern, Vincent Kompany, alisema timu yake iko tayari kwa changamoto ya nusu fainali dhidi ya PSG. “Tunaamini zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Tulipambana hadi mwisho bila kukata tamaa dhidi ya Real Madrid, na sasa tuko tayari kwa hatua inayofuata,” alisema Kompany.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.