Barcelona Yakaribia Kumsainisha Mkataba Mpya Hansi Flick

Utawala wa kocha Hansi Flick ndani ya klabu ya FC Barcelona unatarajiwa kuendelea baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano ya mdomo ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi, hatua inayolenga kuendeleza mafanikio ya klabu hiyo.

Barcelona Yakaribia Kumsainisha Mkataba Mpya Hansi FlickFlick, ambaye mkataba wake wa sasa ungemalizika mwaka 2027, ameendelea kuwa mhimili muhimu katika kurejesha ubora wa Barcelona tangu alipoteuliwa kuinoa timu hiyo katika msimu wa 2024/25.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika msimu wake wa kwanza, Flick aliiongoza Barcelona kutwaa mataji matatu makubwa ikiwemo La Liga, Copa del Rey, na Supercopa de España, huku pia akiiwezesha timu kumaliza msimu kwa ubabe mkubwa dhidi ya wapinzani wao wa jadi.

Barcelona Yakaribia Kumsainisha Mkataba Mpya Hansi Flick“Flick ameleta mabadiliko makubwa katika falsafa ya timu na matokeo yake yanaonekana wazi uwanjani,” kilisema chanzo cha ndani ya klabu hiyo. Barcelona pia ilifanya vyema dhidi ya Real Madrid kwa kushinda mechi zote nne za El Clásico msimu uliopita, ikiwa ni pamoja na ushindi mkubwa wa 4-0 ugenini katika uwanja wa Santiago Bernabéu.

Barcelona Yakaribia Kumsainisha Mkataba Mpya Hansi FlickChini ya uongozi wake, Barcelona imekuwa moja ya timu hatari zaidi barani Ulaya kwa mashambulizi, ikiwa imefunga zaidi ya mabao 100 katika msimu mmoja wa ligi, huku ikiendelea kutetea ubingwa wa Supercopa de España msimu wa 2025/26, ishara ya mwendelezo wa mafanikio yake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.