Kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick, amesema anafurahia kuinoa klabu hiyo lakini hana haraka ya kupata majibu kuhusu hatma yake, huku timu hiyo ikikaribia kufuzu michuano ya UEFA Champions League.
Carrick, aliyewahi kuwa kiungo wa United, aliteuliwa kushika nafasi ya ukocha hadi mwisho wa msimu baada ya kuondoka kwa Rúben Amorim mwezi Januari kufuatia mzozo wa ndani ya klabu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Tangu achukue jukumu hilo, Carrick ameiongoza timu hiyo kupata ushindi muhimu dhidi ya Manchester City na Arsenal, matokeo yaliyoisogeza United hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Premier League.
“Nimesema mara nyingi, ninafurahia kuwa hapa na ninaipenda nafasi niliyonayo,” alisema Carrick Alhamisi kuelekea mchezo wa Jumatatu dhidi ya Brentford.
“Tumeanza kupata matokeo mazuri na bado tuna nafasi ya kuboresha zaidi. Kuna mambo mengi bado tunahitaji kufikia,” aliongeza, akisisitiza kuwa timu inaendelea kujijenga hatua kwa hatua.
Kuhusu mustakabali wake, Carrick alisema hana presha ya kutaka majibu ya haraka. “Kwa kweli sihisi kama ninahitaji kufuatilia muda maalum. Mambo yatakuwa wazi wakati sahihi utakapofika,” alihitimisha kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England.

