Alessandro del Piero: Mtoto wa Fundi Umeme aliyeisimamisha Madrid Santiago Bernabeu

Turudi nyuma kwanza hadi November 9 1974 pale Conegliano Italy, mama mfanya kazi wa ndani na baba fundi umeme walijaliwa mtoto wa kwanza mwanaume na kumuita jina la kiitaliano Alessandro. Mzee Del piero alimuita mwanawe jina hilo akiamini atazunguka duniani akiwa dereva wa magari sababu hawakuwa na kipato kikubwa cha kutosha kumuonesha dunia mwanao, kama ilivokuwa ndoto zao.

Ila laiti kama wangejua miguu ya mtoto wao huyo ilikuwa imebeba maajabu ya kubadilisha maisha yao labda wangemuita jina la kishujaa zaidi kama Fransesco, Thiago au Antonio. Ila jina halikuwa kitu kwani wazazi wake na dunia walishuhudia Alesandro akiwa shujaa wa mpira na si msafirishaji kama walivodhani.

Delpiero


Allesandro alianza kuonesha maajabu utotoni alipokuwa akicheza na watoto wenzake nje kidogo ya soko ambapo ndipo yalipokuwa makazi yao. Uhodari wake wa kukaa na mpira mguuni ulimfanya kuwa maarafu sana mjini Conegliano hadi kupelekea kusajiliwa na Club ya Padova iliyokuwa inashiriki Serie B wakati huo..

Mwaka mmoja tu alishaonekana lulu na vilabu vikubwa vikatamani kupata huduma yake. Alijiunga na Juventus 1993 na hapa ndipo alipoutangaza uwezo wake wa kuuchezea mpira.

Misimu yote 19 aliyovaa jezi ya Juve hawakuwahi kujua Del piero ni mzuri zaidi nafasi gani uwanjani. Hiyo ilitokana na uhodari wake wa kucheza kwa ufasaha sehemu nyingi za ushambuliaji.

Ukienda Italy kuna goli moja maarafu linaitwa “del piero goal” mchezaji akitokea kwenye flank akipiga chenga alafu anapofika karibu na box anafunga kwa kuupiga mpira kwenye corner ya juu ya goli watangazaji hawateseki kusimulia wanasema tu he has scored a del piero. Magoli ya aina hiyo aliyafunga sana hadi yakabatizwa kwa jina lake.

Mashabiki wa Real Madrid wanasifika kwa kiburi na majivuno. Ila haikuwa hivo mbele ya Del piero. Mwaka 2008 Juventus walipokuwa wanacheza na Madrid pale Santiago bernabeu Del piero alikuwa kitanzi kwa Madrid usiku huo. Aliwafunga goli mbili. Wakati anatoka mashabiki wa Madrid walisimama wakampigia makofi wakiimba Del piero. Waliamini yeye ni mmoja wao. Walisema hapa wamepita mafundi ila na wewe ni zaidi.

3 Komentara

    Nice update 👍

    Jibu

    Hongera Sana

    Jibu

    Pongezi sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.