Taarifa mablimbali zisizo rasmi zinasema vigogo wawili wa Soka la Bongo, Simba na Yanga wako vitani kuwania saini ya beki kitasa kutoka Congo, Hennock Inonga maarufu kama Varane.

Klabu ya Yanga walikuwa wa kwanza kuhusishwa na mchezaji huyu lakini baadae Simba wakaingilia dili hilo. Kwa lugha za kwenye vibanda umiza ni kwamba Yanga wamebipu, Simba wamepiga.
Habari za chini ya kapeti zinasema, kitendo cha Yanga juzi kutishia kwamba wamemsajili Peter Banda kiliwakera mabosi wa Simba na wakaapa kuwa watapiga kwenye mshono.
Usiku wa kuamkia jana wamemshusha nchini beki Mkongoman, Hennock Inonga ‘Varane’ ambaye Yanga walishamtumia kila kitu mpaka tiketi, malipo ya cheti cha corona ili aje Dar atue Jangwani.
Simba ilikuwa ikiwinda beki mzoefu kwani matarajio yao ni kufanya vyema katika Ligi ya Mabingwa inayoanza mwezi ujao Septemba na hapo imemnasa Hennock ambaye alikuwa nahodha wa DC Motema Pembe na timu ya taifa ya DR Congo kwa wachezaji wa ndani.
Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!



Sania+mapua
Tunamsubiri kwa hamu huyo Varane wa congo