Kulingana na mwandishi wa habari za michezo Fabrizio Romano, Klabu ya Arsenal bado inavutiwa kutaka kumsajili mchezaji wa Lyon Houssem Aouar.
Gunners ilishindwa kufikia makubaliano na kiungo huyo msimu uliopita wa kiangazi, lakini Aouar sasa anapatikana kwa dau dogo la angalau pauni milioni 20.
“Kuna hali ngumu kwa upande wa wakala, na ndio sababu tutamuona Aouar hadi siku za mwisho ya dirisha kwa sababu sasa bado kuna tetesi kwa klabu kadhaa ambazo ni Tottenham na Arsenal,” alisema kwenye kituo cha Youtube cha Don Robbie.
“Klabu hizi mbili zina nia ya kweli kwa Aouar. Arsenal kama unavyojua vizuri walimtaka na bado wanaangalia hali yake. Lakini sasa ni muhimu kwa Gunners kuuza wachezaji. ”
Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.


