Klabu ya Chelsea ipo katika mipango yake ya kuhakikisha wanakamilisha dili la kumsajili mlinzi wa kifaransa kutoka Sevilla, Joules Kounde baada mchezaji huyo kukubaliana maslahi binafsi na klabu.
Kulingana na Sportitalia, Pamoja na Chelsea kuona dau la kwanza likikataliwa na Sevilla, Bluez wamepeleka dau jingine la €60m (£51.4m) kupata saini ya Jules Kounde.
Wakati huo pia Chelsea inataka kumuuza mlinzi mwingine wa kifaransa Kurt Zouma kuelekea West Ham ili kuacha nafasi ya Kounde kutua Stamford Bridge.
Kulingana na muandishi wa habari za michezo Jack Rosser, Kurt Zouma atafanya vipimo vya afya leo jijini Paris katika usajili wa kuelekea West Ham kwa ada ya £25million.
Makubaliano binafsi yameshafanyika na mawakala wa Zouma, 26 akitajwa kupewa mkataba wa miaka 5 na mshahara wa £125,000 kwa wiki.
Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.



Issa
The blues moto