Meneja wa Rangers, Steven Gerrard amesema hajashangazwa na taarifa za kubaguliwa kwa mchezaji wake, Glen Kamara kutoka kwa watoto wa shule katika mchezo wa Europa League.

Kamara alizomewa na mashabiki kila aliposhika mpira zaidi ya mchezaji yoyote wa Rangers, wakati Sparta Prague walipo shinda 1-0 nyumbani.
Tabia hiyo inajitokeza tena ikiwa imepita miezi mitano tangu beki wa Slavia Prague, Ondrej Kudela kufungiwa mechoi 10 baada ya kukutwa na hatia ya kumtolea maneno ya kibaguzi Kamara.
“Alipooulizwa kuhusu tukio hilo Meneja, Steven Gerrard alisema, “Wakati wa mchezo, sikuwa natambua. Nilikuwa nimejikita kwenye mchezona mabadiliko ya mbinu nilizokuwa na fikiria kuhusu kujaribu kuturudiha mchezoni.
“Kama kuna ukweli kuhusu hilo, basi inakatisha tamaa sana, lakini sijashangazwa.” aliongeza Gerrard.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


