Taifa Stars Yakubali Kipigo Dhidi ya Benin.

 

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imekubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya wageni Benin katika mchezo wa kufuzu kucheza kombe la Dunia ulioanza majira ya saa 10 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Taifa Stars ilianza vizuri katika kipindi cha kwanza huku wakitengeneza nafasi nyingi za wazi na kushindwa kuzitumia, ikiwemo nafasi ya dhahabu aliyoipata mshambuliaji wa Wydad Casablanca, Saimon Msuva.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi timu zote zikitafuta nafasi ya kuongoza. Ni Benin ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Stars baada ya Steve Mounie kupiga shuti la ufundi lililompita beki na kipa Aishi Manula katika dakika ya 71′ ya mchezo.

Mpaka dakika 90 zinakamilika, Benin wanaibuka na alama 3 ugenini licha ya Taifa Stars kufanya mashambulio kadhaa dakika za mwisho ambazo hazikuzaa matunda.

Benin wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 7 wakifuatiwa na Congo wenye alama 5 baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Madagascar, Stars akiwa nafasi ya tatu na alama 4 na Madagascar akishikilia mkia katika kundi J.


SPACE SPIN NA MERIDIANBET.

Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.