Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford ametunukiwa tuzo ya juu zaidi ya heshima inayotolewa na Chuo kikuu cha Manchester na kuweka rekodi ya kuwa kijana mwenye umri mdogo zaidi kutunukiwa tuzo na Chuo hicho.

Marcus mwenye umri wa miaka 23 ametunukiwa tuzo hiyo kwa kufanya mambo yanayoigusa Jamii ikiwemo kuwasaidia watoto waishio kwenye mazingira magumu katika shule mbalimbali kupata chakula wakiwa mashuleni.
Hafla hiyo imefanyika Old Trafford kwenye dimba la Man United na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Sir Alex Ferguson.
Harakati za mchezaji huyo zinakubalika na wengi na miezi michache iliyopita, Dr. Rashford alizungumza pia na Rais Obama.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


