Saudi Arabia Public Investment Fund wamekamilisha umiliki wa klabu ya Newcastle United kutoka kwa Mike Ashley kwa dau la Pauni Milioni 300.

Premier League imedhibitisha ununuzi wa klabu hiyo siku ya jana na kusema wamepokea uhakika wa kisheria kwamba Ufalme wa Saudi Arabia hautadhibiti Newcastle United.
Habari za ndani za klabu hiyo zinasema, wamiliki hao wapya wanampango wa kubadili kocha wa sasa Steve Bruce kama kocha mkuu, lakini maamuzi hayo bado hayajafanywa.
Wamiliki wapya wa Newcastle, wanaomiliki Public Investment Fund (PIF), PCP Capital Partners na RB Sports & Media wana utajiri mara 10 wa tajiri wa Man City Sheikh Mansour Bin Zayed.
Mchezo unaofwata wa Newcastle United utakua dhidi ya Tottenham, tarehe 17 Oktoba na taarifa katika klabu hiyo zinasema tiketi zote kuelekea mchezo huo utakao kuwa wa kwanza kwa mmiliki mpya.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


