Nyota wa Ajax ambaye ni nahodha wa klabu hii Matthijs de Ligt amepania uhamisho wa kwenda Barcelona mwisho wa msimu, atamfuata De Jong!
Nyota huyu kinda anachukuliwa kama mmoja wa walinzi bora zaidi duniani akiwa na miaka 19 tu. Staa huyu anatajwa kuwepo kwenye rada ya Barcelona na baadhi ya klabu zingine kubwa duniani.
Barcelona ambao tayari wamekamilisha usajili wa mchezaji mwenzie na De Light, Frenkie de Jong atakayetimkia kwenye soka la Hispania msimu ujao wa Joto bila shaka wanahitaji kumvuta na huyu mlinzi bora ambaye bado ni kinda kabisa.
Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, De Ligt anataka kumfuata De Jong pale Camp Nou msimu huu unapoisha. Barcelona watahitaji kulipa, paundi milioni 65 na nyongeza ya paundi milioni 9 ili kumsainisha kinda huyu.
Juventus walikuwa wanahusishwa na nyota huyu, kwa mujibu wa Tuttorsport siku kadhaa zilizopita Juventus walikuwa wanamatumaini kwa watashinda mbio za kumnasa kinda huyu kutoka Ajax.
Klabu nyingine inayoungana na Barcelona na Juventus kwenye mbio hizi ni Manchester City. Kama De Light anapendelea zaidi kujiunga na Barcelona basi Juve na Man City tayari wana nafasi finyu zaidi, wataweza kumpata kama Barcelona wakishindwa kumchukua.


Povel
Habar njema
Furahav
Iko vizuri.
Lydia Emmanuel Magoti
Iko vizuri