Meneja wa Klabu ya AS Roma, Jose Mourinho amekataa kujibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kipigo cha 3-0 nyumbani dhidi ya Inter Milan katika mchezo wa Ligi ya Italia, Serie A.

Mourinho alisisitiza kuna sababu za wao (makocha) kulipwa zaidi kuliko waandishi wa habari mara tu baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Kocha huyo asiyeishiwa vituko aligoma kabisa kuzungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo huku akiwa amekasirika.
“Kazi yenu ni rahisi zaidi zaidi yetu na ndio sababu tunalipwa zaidi kuliko nyinyi, “alisema meneja huyo wa AS Roma baada ya mwandishi wa habari kutaka kuuliza swali.
Katika maongezi yake Mourinho alisema, “Tunaomba ladhi studio, na watu waliko nyumbani ambao walikuwa wanatamani maswali yao.
“Inter ni bora kuliko sisi katika hali ya kawaida. Na katika hali isiyo ya kawaida walikua bora zaidi yetu. Msimu uliopita, walikuwa alama 29 mbele ya Roma. Leo tukiwana majeruhi na wwachezaji walisimamishwa, ilikuwa ni ngumu, ngumu sana.
“Safu yetu ya ushambuliaji ilikuwa sawa na sifuri. Ilikuwa ni muhimu kufunga goli, kwasababu tulikuwa na nafasi mbili au tatu. Tulikuwa na nafasi tatu tukashindwa kuzitumia.” aliongeza.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


