Simba SC Yavunja Mkataba na Hitimana.

 

Klabu ya Simba SC hapo jana imetangaza kuvunja mkataba na kocha msaidizi Thierry Hitimana baada ya kudumu na klabu hicho chini ya miezi mitatu.

Taarifa hizo zimekuja ghafla siku chache baada ya ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya KMC mjini Tabora. Ikumbukwe Hitimana aliwahi kusimama katika mechi mbili za mashindano ya Afrika baada ya kocha mkuu kukosa vigezo.

“Uongozi wa Klabu ya Simba SC umefikia makubaliano na pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Msaidizi Thierry Hitimana, kuanzia jana Desemba 28, 2021.

Simba SC inamshukuru Hitimana kwa mchango wake aliotoa kwa timu tangu alipojiunga nasi na tunatakia kila la kheri katika maisha yake popote aendako.” imeandika taarifa hiyo.

Simba SC itacheza mechi inayofuata dhidi ya Azam FC siku ya January 01, 2022 ikiwa na kocha mkuu Pablo na kocha msaidizi Suleiman Matola.


KUWA MILIONEA MSIMU WA SIKUKUU NA SAHARA RICHIES

Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.