Ukimuangalia usoni, ni kama mtu mstaarabu flani lakini, Pep Guardiola sio mtu wa mchezo mchezo. Anahasira na maamuzi magumu akiamua kuwa hivyo.
Hili linajidhihirisha kupitia Kyle Walker. Beki wake tegemezi kwenye upande wa kulia lakini, alijichanganya kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya RB Leipzig.
Huu ni mchezo ambao Walker alicheza rafu mbaya kwa Andre Silva ambapo, amejikuta akifungiwa kucheza michezo 3 ya Ligi hiyo. Hiki sio kitu ambacho Pep anakihusudu kwa namna yeyote.
Kimsingi, Guardiola bado anahasira na Walker kwa kitendo alichokifanya kwenye mchezo ule. Licha ya kuwa City wameshaweka mguu mmoja kwenye hatua ya robo fainali baada ya ushindi wa goli 5 dhidi ya Sporting Lisbon, kumkosa Walker kwa sababu ya kucheza rafu, ni kitu ambacho Guardiola hawezi kukifumbia macho hata kidogo.

Mchezaji anapofanya kitu cha kipumbavu, anastahili kufungiwa michezo mitatu. Siwezi kuwa mstaarabu kwa Kyle kwa tukio kama hili, bado ninahasira na yeye
Anachokisema Guardiola ni anakimaanisha. City walitaka kukata rufaa ya kutokukubaliana na uamuzi huo lakini, Pep alipinga juhudi za City akiamini kuwa, japo wachezaji wengine waliowahi kufanya matukio kama hayo walifungiwa michezo 2, Walker amestahili kufungiwa michezo 3.
Walker alifanya tukio hilo wakati ambao Man City walikua wanaongoza kwa magoli 5 zikiwa zimesalia dakika chini ya 10 mchezo kumalizika.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


