Zirkzee Aongezwa Kwenye Kikosi cha Uholanzi Kwaajili ya EURO 2024

Mshambuliaji wa Bologna Joshua Zirkzee ameitwa kwenye kikosi cha Uholanzi kwa ajili ya EURO 2024 baada ya kiungo wa Atalanta Teun Koopmeiners kujiondoa kutokana na jeraha.

Zirkzee Aongezwa Kwenye Kikosi cha Uholanzi Kwaajili ya EURO 2024
Mshambuliaji huyo awali aliachwa na kocha Ronald Koeman kwa mchuano huo utakaong’oa nanga kesho nchini Ujerumani.

Uholanzi iko katika kundi moja na Ufaransa, Poland na Austria. Ndugu mteja usisahau kubeti na Meridianbet  ambao ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Wamekuwa na matatizo mengi ya majeraha, kwani mshambualiaji wa Ajax Brian Brobbey pia anatatizo la kuwa fiti kwa mchezo wa kwanza.

Kiungo wa kati wa Atalanta Koopmeiners alilazimika kujiondoa kutokana na jeraha la misuli, kama alivyofanya mchezaji mwenzake wa klabu Marten de Roon.

Zirkzee Aongezwa Kwenye Kikosi cha Uholanzi Kwaajili ya EURO 2024

Sasa Koeman amemuongeza Zirkzee kwenye kikosi kama mbadala wa Koopmeiners, ingawa wanacheza katika majukumu tofauti kabisa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hana hata mechi moja ya wakubwa chini ya ukanda wake wa Uholanzi, lakini alifunga mabao saba katika mechi 19 alizocheza kwa timu ya U-21.

Zirkzee alifunga mabao 12 na kutoa asisti saba katika mechi 37 za kimashindano akiwa na Bologna msimu huu na yuko kwenye mazungumzo na Milan, pamoja na Juventus, Arsenal na Manchester United.

Acha ujumbe