Uingereza: Kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza michezo ya ligi ya Uingereza kuahirishwa hii leo kwa ishara ya heshima kwa Malkia huyo.  Mechi mbalimbali zilitakiwa kuendelea leo siku ya Ijumaa.

 

https://app.mrdn.co/bashiri01

Malkia huyo alifariki hapo jana nyumbani kwake Balmoral akiwa na umri wa miaka 96 huku akiwa amekalia kiti hicho kwa miaka 70 tangu atawazwe kuwa Malkia akiwa na umri wa miaka 27 na sasa nafasi hiyo inachukuliwa na mwana wa mfalme Charles wa tatu.

Ligi hiyo ya Daraja la kwanza Norwich walikuwa na ratiba ya kukipiga dhidi ya Burnley siku ya leo, huku Tranmere Rovers na Stockport zikipangwa kukutana katika ligi ya pili. Sasa michezo yote miwili imesitishwa huku EFL ikitibitisha kuwa uamuzi utafanywa kwenye michezo iliyosalia ya wikend siku ya Ijumaa .

 

Ligi ya Uingereza Kuahirishwa leo

Taarifa kwenye tovoti ya EFL ilisema kuwa:

Ikiwa na ishara ya heshima, kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth wa pili mapema leo hii, mechi iliyopangwa kuchezwa kesho (Ijumaa Septemba 9) Burnley vs Norwich, na  Tranmere Rovers vs Stockport zimehairishwa. 

Ratiba ya ligi itapangwa lini itachezwa ila kwa ratiba ya michezo ya kesho itaendelea kama kawaida pale Uingereza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa