Kikosi cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Aprili 9 2025 kiliandika rekodi ya kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa penati 4-1 baada ya dakika 90 za pili ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 2-0 Al Masry.

Fadlu kabla ya mchezo aliweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kupata ushindi na kuzuia kutofungwa ndani ya dakika 90 jambo ambalo wachezaji walitimiza kwa ushirikiano ndani ya dakika 90, safu ya ulinzi chini ya Hamza Jr ilifanya kazi kubwa kwa ushirikiano na Zimbwe Jr ambaye ni nahodha, Shomari Kapombe Legend wa muda wote Simba.
Katika dakika 45 za mwanzo Simba waliwanyanyua mashabiki wao kupitia kwa Ellie Mpanzu dakika ya 22 na Steven Mukwala dakika ya 32 na ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza Uwanja wa Suez Canala ulisoma Al Masry 2-0 Simba hivyo mshindi alitafutwa kwa penati.
Mukwala alipachika bao la pili kwa pigo la kichwa akitumia krosi iliyotoka kwenye mguu wa beki wakupanda na kushuka Mohamed Hussein Zimbwe Jr ambaye alikuwa kwenye majukumu yake kama Camara ambaye alifanya kazi yake kuzuia mpira usiguse nyavu za Simba.



