PACOME: SASA KILA MECHI NI FAINALI

Pacome Zouzoua kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kila mechi ni ngumu wakiwa uwanjani wanapambana kufanya vizuri kupata matokeo ndani ya uwanja.

PACOME: SASA KILA MECHI NI FAINALI

Aprili 2 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ulisoma Tabora United 0-3 Yanga, mabao ya Israel Mwenda, Clement Mzize na Prince Dube yalitosha kuipa pointi tatu Yanga.

Pacome alitoa pasi kwa Mzize dakika ya 56 kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 ikaleta bao la pili baada ya shambulizi la kushtukiza na alitoa pasi ya pili kwa Dube dakika ya 67 akiwa nje ya 18 kwa mguu wake wa kulia hali iliyopelekea kuhusika kwenye mabao mawili kati ya matatu.

Yanga inakuwa ni timu namba moja kufunga mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 61 na safu washambuliaji wake wawili Mzize na Dube kila mmoja katupia mabao 11 kwenye ligi.

PACOME: SASA KILA MECHI NI FAINALI

Pacome anafikisha jumla ya pasi 8 za mabao ndani ya ligi akiwa ni namba mbili kwa mastaa wenye pasi nyingi huku kinara akiwa ni Feisal Salum wa Azam FC mwenye pasi 12 kibindoni.

Kiungo huyo amesema: “Kazi bado inaendelea furaha kubwa kuona kwamba tunapata ushindi kwani mchezo wetu dhidi ya Tabora United hakuwa mwepesi tulikutana na timu ngumu yenye wachezaji wazuri.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.