Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibengé, amesema kuwa sare mbili mfululizo ambazo timu yake imezipata katika michezo ya ugenini hazijapunguza dhamira ya klabu hiyo kuendelea kupigania ubingwa wa Tanzania Premier League msimu huu.

Ibengé ameleza kuwa licha ya matokeo hayo, kikosi chake bado kina nafasi kubwa ya kufikia malengo yao kutokana na idadi ya michezo iliyobaki kwenye ligi. Alisisitiza kuwa wachezaji wake wanaendelea kupambana kwa nguvu na wana ari ya kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika michezo ijayo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo pia amekiri kuwa changamoto kubwa ambayo imejitokeza kwa sasa ipo katika eneo la ushambuliaji, hasa katika kutumia nafasi za kufunga mabao ambazo timu imekuwa ikizipata ndani ya uwanja.
Hata hivyo amesema atafanya kazi ya ziada katika mazoezi ili kuhakikisha washambuliaji wa timu hiyo wanaongeza umakini na makali mbele ya lango, jambo litakalosaidia timu kurejea kwenye mwelekeo wa ushindi katika michezo ijayo.

“Bado tuna mechi nyingi za kucheza na hatujapoteza malengo yetu. Tatizo limetokea kwenye kutumia nafasi za kufunga mabao, nitalifanyia kazi. Kiuwezo nawapongeza vijana kwa namna wanavyopambana,” alisema Ibengé.

