Yanga Yapata Ushindi Mwembamba Chamazi

Ligi kuu ya NBC Tanzania hapo jana iliendelea kwa michezo kadhaa ambapo mchezo wa usiku saa 3:00 ulikuwa ni kati ya bingwa mtetezi Yanga vs KMC kule Azam complex ambapo wananchi waliweza kuibuka na ushindi.

Yanga Yapata Ushindi Mwembamba Chamazi

Bao hilo la ushindi lilifungwa mapema kabisa dakika ya 4 na Maxi Nzengeli huku mechi hiyo ikiwa ni kushambulia na kulinda.

Yanga walicheza kikubwa sana kwani kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho walikuwa wanalishambulia lango la KMC ambao wanadhaminiwa na Meridianbet lakini vijana hao wa Moalin walikaa imara.

Mashabiki wengi wa Young Africans walidhani itakuwa ni mechi nyepesi sana kwao kwani mechi ya mwisho walivyokutana katika dimba hilo KMC walipoteza kwa idadi kubwa ya mabao lakini jana ni bao moja pekee.

Yanga Yapata Ushindi Mwembamba Chamazi

Licha ya Gamondi kufanya mabadiliko ya wachezaji kama vile Mzize, Kennedy Musonda, Duke Abuya na wengine wengi lakini bado ilikuwa ngumu. Kwa upande wa KMC Lanso ndiye alifanya kazi kubwa ya kuwazuia Yanga kufunga mabao kutokana na kiwango alichokionyesha jana.

Mechi inayofuata, vijana wa Gamondi watakipiga dhidi ya Pamba, huku Wanakino boys wao watawaalika Kagera Sugar.

Acha ujumbe