Ligi kuu ya NBC Tanzania itaendelea hii leo kwa mchezo mmoja ambapo klabu ya Azam FC itakuwa katika dimba la Chamazi Complex kumenyana dhidi ya Tanzania Prisons majira ya saa 1:00 usiku.
Azam wametoka kutolewa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mikwaju ya penati baada ya timu hizo kuwa na aggragate sawa ya (3-3) dhidi ya Bahir Dar Kenema.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Leo hii atakuwa na kibarua kizito dhidi ya Wajela jela nyumbani kwake huku malengo yake yakiwa ni kusaka pointi tatu pekee kwenye mchezo wa leo na mchezo wa kwanza alipata pointi 3 baada ya kumfunga Kitayosce ambayo walikuwa pungufu.
Tanzania Prisons wao mechi ya kwanza ya Ligi walitoa sare na wanashikilia nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi. Wakati Wanalamba lamba wao wapo nafasi ya 5 kwenye msimamo hadi sasa.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Ushindi wa vijana wa Dabo leo hii utawafanya waongoze ligi kwa tofauti ya mabao dhidi ya Simba ambaye kwasasa ndiye anashikilia nafasi hiyo baada ya kuwa na tofauti ya mbao mengi kwenye michezo miwili.
Mechi ya mwisho kukutana kwenye ligi timu hizi zote mbili, Prisons alipoteza mchezo huo akiwa ugenini. Hivyo leo hii anataka kulipiza kisasi , ataweza mbele ya Matajiri hawa wa Chamazi?