AZAM FC MIPANGO INAKWENDA SAWA KABISA

KOCHA Mkuu wa Azam FC Youssouph Daho raia wa Senegal Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa matokeo ambayo wanayapata kwenye mechi za kirafiki sio muhimu kikubwa ni kupata majibu wa kile wanachokitafuta.

Timu hiyo imeweka kambi Tunisia ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2023/24 ikiwa inacheza na mechi za kirafiki inatambua kwamba mabingwa ni Yanga msimu wa 2022/23.AZAM FCWikiendi iliyopita ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya US Monastri mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwa timu hiyo.

Dabo amesema kuwa anafurahishwa na uwezo wa wachezaji wake namna unavyoimarika huku wakizidi kujipanga kupata kilicho bora zaidi.

“Kwa namna ambavyo wachezaji wanacheza wanaonyesha kuna kitu hivyo hatuangalii matokeo bali tunaangalia kile ambacho kitatufanya tuwe bora,”.

Azam FC ina kazi ya kuanza kwenye Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mchezo wao dhidi ya Yanga ni wa ufunguzi wa msimu mpya wa 2023/24 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.AZAM FCIkumbukwe kwamba mabingwa wa msimu wa 2022/23 wa Ngao ya Jamii ni Yanga waliwatungua Simba.

Kwenye droo ya kimataifa Azam FC ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika imepangwa kumenyana na Bahir Dar Kenema FC ya Ethiopia katika Raundi ya Kwanza ya mchujo ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).

Acha ujumbe