Klabu ya Azam FC wamefanya usajili wa kocha mkuu anayejulikana kwa jila la Youssouph Dabo kutoka Senegal kwa ajiili ya kuinoa timu hiyo kwa mkataba wa miaka 03 kuanzia msimu ujao.
Dabo ni raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 43 na uzoefu kwenye soka la Afrika.
Dabo amewahi kuwa kocha wa mchezaji wa Simba SC, Pape Ousmane Sakho wakati akiitumikia Tengueth FC ya Senegal pamoja na Malickou Ndoye beki anayecheza Azam FC kwa sasa.
Amewahi pia kufundisha klabu ya Jaraaf FC na hapo awali Stade de Mbour na Guediawaye zote za Senegal.
Kocha huyo pia amewahi kuifundisha timu ya taifa ya Senegel ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ( Senegal U20 )



