Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara iliendelea kwa michezo miwili hapo jana ambapo mchezo wa mwisho kabisa uliopigwa majira ya saa 3:00 usiku ulikuwa ni kati ya Azam Fc dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mechi hiyo ilikuwa ya wazi kwa pande zote mbili huku kila timu ikishambulia lango la mwenzake kwa wakati ili kupata bao la kuongoza licha ya Azam Fc kupata mkwaju wa penalti lakini walishindwa kuutumia vizuri baada ya Idris Mbombo kukosa.
Baadae wakaja kujipatia bao la kuongoza kupitia kwa Issa Ndala dakika ya 39 kabla ya Idd Selemani Naddo kutokea benchi na kupachika bao la pili amablo lilikuwa ndilo la ushindi.

Mtibwa nao hawakukaa nyuma wakajipatia bao moja kupitia kwa mchezaji wao Mayaya dakika 15 kabla ya kumalizika kwa mchezo huo na kuwafanya washikilie nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi.
Baada ya ushindi huo Azam FC amebaki nafasi ile ile ya 4 akiwa na pointi zake 50 tofauti ni pointi 1 pekee na aliyeko nafasi ya 3 ambaye ni Singida Big Stars mwenye pointi 51 baada ya kushinda jana.

