Azam Kuzichapa na Malimao FC Leo

Klabu ya Azam FC inatarajia kumualika Malimao FC kutoka mkoani Katavi kwaajili ya mchezo wao wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) utakaopigwa majira ya saa 1:00 usiku.

 

Azam Kuzichapa na Malimao FC Leo

Mchezo huo wa Azam dhidi ya Malimao utapigwa katika uwanja wa Chamazi Complex huku kaimu kocha mkuu wa Wanalambalamba Kali Ongala akisema kuwa wamejiandaa vyema kushinda mechi hiyo.

Timu hiyo imekuwa kwenye ubora mkubwa sana toka timu hiyo ipate kocha huyo kwani mpaka sasa wamecheza mechi 8 bila kupoteza mechi zote wala kutoa sare, bali wameshinda zote.

Wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa NBC wakiwa wamejikusanyia pointi zao 35 baada ya kucheza michezo yao 15 ya mzunguko wa kwanza na sasa wanatarajia kushinda mechi yao ya leo.

Azam Kuzichapa na Malimao FC Leo

Msimu uliopita walitolewa hatua ya nusu fainali na Coastal Union kwa mikwaju ya penalti.

 

Acha ujumbe