Uongozi wa Azam FC umefunguka kuwa hauna mpango wa kumleta kocha Mkuu mpya ndani ya kikosi chao kutokana na matokeo mazuri wanayopata.

Azam Fc waliachana na Kocha wao Mkuu, Denis Lavagne kwa makubaliano ya pande zote mbili na kikosi kunolewa na kaimu kocha Mkuu, Kali Ongala.

Azam hawana mpango na kocha mpya

Ongala tangu akichukue kikosi hicho, amefanya vizuri ambapo mpaka kumalizika kwa mechi 15 za mzunguko wa kwanza timu hiyo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Azam hawana mpango na kocha mpya

Akizungumzia hilo, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema “Hatuna haja ya kumpa kocha mkataba mpya kwani ana mkataba mrefu.

“Mpango wa kumleta kocha mpya kwa sasa hatuna kutokana na matokeo mazuri ambayo tunayapata lakini ikitokea mfululizo wa matokeo mabaya tungemleta kocha mpya.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa