Aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique ametangaza rasmi kuachana timu hiyo punde tu baada ya Hispania kutupwa nje kwenye michuano ya kombe la dunia dhidi ya timu taifa ya Morocco.
Baada ya kikao cha ndnani baina ya kocha huyo na shirikisho la soka nchini Hispania wamefikia makubaliano na ni rasmi ndoa ya kocha huyo na timu ya taifa ya Hispania imevunjika rasmi baada ya kudumu kwa muda wa miaka takribani minne.Kocha Enrique amefanikiwa kwa kipindi cha miaka minne alichokaa kwenye timu ya taifa ya Hispania baada ya kufanikiwa kuingia Nusu fainali ya michuano ya Uefa Nations League mara mbili,fainali ya michuano hiyo mara moja, Na Nusu fainali ya michuano ya Euro mwaka 2020.
Kocha huyo amefanikiwa kutengeneza timu ya taifa ya Hispania huku akiwapa vijana wadogo nafasi kwenye kikosi cha timu hiyo wachezaji kama Pedri,Gavi, Balde ni baadhi ya vijana ambao hawajavuka miaka 20 ambao wamefanikiwa kuitwa kwenye timu ya taifa ya Hispania chini ya kocha huyo.Kocha Luis Enrique amaye amewahi kua kocha wa klabu ya Barcelona akifanikiwa kuwapa mataji matatu kwa msimu mmoja kwasasa inaelezwa kocha huyo anapanga kurudi kwenye ngazi ya klabu kwa mara nyingine tena.