Nusu fainali ya kwanza ya Mapinduzi CUP inatarajiwa kupigwa leo majira ya saa 2:15 usiku ambapo mabingwa mara nyingi Azam FC watamenyana dhidi ya Singida Big Stars kuwania kucheza fainali.
Azam FC inahitaji hili Kombe baada ya kuona kuwa kugombea taji la ligi kuu ni vigumu kutokana na pointi alizozidiwa na kinara wa Ligi Yanga lakini pia na anayeshika nafasi ya pili Simba.
Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Amani ambapo pia kwa upande wa Singida nao wanahitaji angalau wachukue Kombe hili kwani kwenye Ligi napo ni ngumu kuchukua kutokana na ushindani uliopo kwa vilabu vikubwa.
Singida na Wanalamba Lamba wameshakutana kwenye Ligi na Azam akaibuka na ushindi mwembamba. Je Leo hii walima alizeti watakubali kupoteza mara nyingine kwa matajiri wa Chamazi?