Ligi kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kupigwa hii leo kwa mechi moja kwenye majira ya saa 10:00 jioni ambapo Coastal Union watawaalika Dodoma Jiji katika Uwanja wao wa Mkwakwani.

 

Coastal Union Dhidi ya Dodoama Jiji ni Leo

Coastal mpaka sasa amecheza michezo 7, ameshinda michezo miwili, sare mbili na amepoteza michezo mitatu huku akiwa amejikusanyia pointi 8. Wakati kwa upande wa Dodoma Jiji yeye amecheza michezo 9, kashinda mmoja, sare tatu na kapoteza mara 5, alama sita mpaka sasa.

Wagosi wa kaya mechi yao ya mwisho walitoa sare ya bila kufungana dhidi ya Geita Gold, wakati Dodoma pia wakitoa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi wakiwa ugenini baada ya kufungwa mapema sana.

Coastal Union Dhidi ya Dodoama Jiji ni Leo

Mechi ya mwisho kukutana Coastal na Dodoma Jiji, Wagosi walijichukulia pointi tatu muhimu kwa walima zabibu hao kwa kumtandika mabao 2-1, wakiwa nyumbani kwao huko Tanga.

Sasa wanakutana mara nyingine tena huku wote wakiwa na uhitaji wa pointi tatu vilevile wakiwa na hali mbaya kwani mwenyeji yupo nafasi ya 13 mpaka sasa na mgeni yupo nafasi ya 15 huku tofauti ya pointi ikiwa ni 2 tu.

Coastal Union Dhidi ya Dodoama Jiji ni Leo

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa