Wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa wanawake Simba Queens leo watashuka dimba la Grand Stade De Marrakech kwaajili ya mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 10:00 usiku kwa majira ya Tanzania, ndiyo utakaoamua hatma ya Simba Queens kama watafuzu hatua ya nusu fainali au wataondolewa na wapinzania wao, ambao wanahitaji sare ya aina yeyote kufuzu tofauti na Simba wanaohitaji ushindi wa aina yeyote.

 

Simba Queens Kuisaka Nusu Fainali Leo

Mchezo wa kwanza wa Simba alipoteza dhidi ya wenyeji AS FAR kwa bao 1-0, na kuwafanya kupoteza alama tatu muhimu ambazo zingewafanya wawe kwenye eneo zuri, lakini kwenye mchezo wa pili walijipapatua na kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Determine Girl kutokana nchini Liberia.

 

Simba Queens Kuisaka Nusu Fainali Leo

Kocha Mkuu wa Simba Queens Charles Lukula alisema kuwa wamejiandaa vya kutosha kupambana ndani ya uwanja ili kupata matokeo, na mchezo huo upo kwa kila upande.

Tayari mwenyeji wa mashindano hayo AS FAR ameshafuzu kwani ana alama 6 mpaka sasa, na leo atacheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Determine Girl ambayo haijashinda mchezo hata mmoja, kwa upande wa kundi B Mamelod Sundowns Queens nao wamefuzu hatua ya nusu fainali.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

Bonyeza hapa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa