KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Yusuph Chipo baada ya kupoteza mechi dhidi ya Ruvu Shooting amewatupia lawama mabeki wa timu hiyo kwa kuruhusu mabao.

Mchezo huo wa ligi kuu ulipigwa jana alhamis kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar ambapo Coastal Union walipoteza kwa mabao 2-1.

 

Kocha Coastal Awatupia Lawama Mabeki

Baada ya mchezo huo kumalizika, Chipo alisema “Kwanza tumshukuru Mungu kwa mchezo kumalizika salama na hakuna mchezaji yeyote mwenye majeraha.

“Kwenye mchezo uliopita mapungufu niliyaona kwenye safu ya ushambuliaji kwani tulitengeneza nafasi nyingi lakini tukazipoteza nilirudi kwenye uwanja wa mazoezi nikalifanyia kazi na leo (jana) umeona tumepata goli la mapema.

 

Kocha Coastal Awatupia Lawama Mabeki

“Kwenye mchezo huu nimeona tena makosa yakifanyika kwenye safu ya ulinzi sasa unaenda kurekebisha mbele na tena huku panavuja lakini nitaenda kulifanyia kazi kwenye kiwanja cha mazoezi ili makosa hayo yasijirudie.”

 

Kocha Coastal Awatupia Lawama Mabeki

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa