Anthony Martial na Marcus Rashford wamerjra mazoezini kuelekea mchezo wao dabi ya jiji la Manchester kati ya klabu hiyo dhidi ya Manchester City.
Wachezaji hao walikua wanatiliwa shaka kutokuepo kwenye mchezo huo siku ya jumapili katika dimba la Etihad lakini leo wameonekana Carrington kiwanja cha mazoezi cha klabu hiyo.
Anthony Martial amekua akisumbuliwa ya majeraha mara kwa mara msimu huu huku Rashford yeye akiwa kwenye kiwango bora kabisa baada ya leo kutangazwa mchezaji bora wa mwezi wa tisa wa ligi kuu Uingereza lakini alikua anahisiwa kukosekana kwenye mchezo huo baada ya kushindwa kuhudhuria mazoezi na wachezaji wenzake.
Anthony Martial amekua ni mchezaji ambae kocha wa klabu hiyo Eric Ten Hag anatamani sana awe na utimamu wa kimwili kwasababu ndio mchezaji ambae anaweza kuweka uwiano kwenye eneo la mbele akicheza kama mtu wa mwusho akicheza kama mshambuliaji wa mwisho.
Marcus yeye amekua na kiwango bora baada ya kua na msaada mkubwa katika mechi nne za mwisho za ligi kuu walizocheza timu hiyo katika ligi kuu ya Uingereza na kufanikiwa kupata ushindi huku mchezaji huyo akihusika kwenye magoli matano kati ya saba klabu hiyo iliofunga.