Klabu ya Coastal Union imeweka wazi hofu yake dhidi ya klabu Yanga kwenye mchezo wao unaotarajia kuchezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, kutokana na ubora wa kikosi cha timu ya wananchi.

Timu hizo zinatarajia kumenyana kesho jumamosi ukiwa ni mchezo wa ligi kuu Bara huku timu zote zikiwa na pointi tatu baada ya kushinda mechi zao za kwanza.

yanga, Coastal Union Yaiogopa Yanga , Meridianbet

Mgunda amesema kuwa: “Tunajua tunaenda kucheza na mabingwa watetezi ni timu ngumu, nzuri ina wachezaji ambao wana uzoefu na benchi la ufundi zuri.

“Kwa kutambua hilo tumejiandaa vizuri kwa kuchukua tahadhari zote ambazo zinapaswa kuchukuliwa kutokana na timu kama hiyo tumezichukua.

“Katika wahanga wa kuondokewa na wachezaji wangu katika kikosi cha kwanza na mimi nipo kwani wameondoka wachezaji saba hivyo kuna ongezeko la zaidi ya wachezaji saba lakini ushindi wa juzi umewaongezea morali wachezaji wangu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa